Mudathir Ashinda Goli Bora Hatua ya Makundi CAF

 


Goli la Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya limeshinda kuwa Goli Bora la Michuano ya Shirikisho Afrika katika hatua ya Makundi baada ya kupigiwa kura na wafuasi wengi kwenye ukarasa wa Twitter wa Shirikisho la Mpira Afrika (CAF).


Goli hilo lilikuwa likishindanishwa na Goli la Aymen Mahious wa USM Alger, Aubin Kouame wa Asec Mimosas na Paul Acquah wa Rivers United.


Goli hilo ni lile alilowafunga TP Mazembe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Kwenye kura zilizopatikana, Mudathir Yahya amepata asilimia 70% ya kura zote zilizopigwa huku Aymen Mahious akipata asilimia 21% na Aubin Kramo akishika nafasi ya tatu Kwa kupata asilimia 5% na nafasi ya nne ikienda Kwa Paul Acquah aliyepata kura asilimia 3% ya kura zote zilizopigwa huko Twitter.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad