Muuguzi afariki akijaribu kufanya upasuaji kupunguza tumbo lake.





Moja ya habari iliyokamata headlines wiki hii ni ripoti iliyoandikwa kupitia jarida la The New York Post, kuripoti kuwepo kwa muuguzi mmoja kutokea Nchini Mexico kufariki baada a kukutwa akiwa amepoteza fahamu katika Ofisi va Daktari baada ya kujaribu kujifanyia upasuaji wa kupunguza tumbo.

Daktari Rolando Samper Mendoza, ambaye ni Mmiliki wa Hospitali hiyo itwayo ‘Clinica Amper’ ya Mexico amesema Mwanamke huyo alijichoma sindano ya ganzi ili kujifanyia upasuaji huo ambao hana nao ujuzi wala uzoefu wowote.

Muuguzi huyo alifariki kwa kupata mshtuko wa moyo muda mfupi baada ya kukutwa na Mfanyakazi mwenzake ambaye aliwapa taarifa Wahudumu wa afya na kujaribu kumsaidia.

Mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Carina, alijaribu kutekeleza upasuaji huo ili kupunguza tumbo lake Hospitalini hapo, kitendo ambacho kilisababisha Muuguzi huyo kujichoma kiasi kikubwa cha ganzi ambayo ilimsababishia madhara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad