Mwanasheria Ataka Wabunge Waliopita Bila Kupigwa Wavuliwe Ubunge



Dar es Salaam. Wiki moja baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu ya kuzuia wagombea nafasi mbalimbali kupita bila kupingwa, mwanasheria Matoja Kosata ameataka wabunge wote walipatikana kwa mtindo huo wavuliwe ubunge wao.

Hukumu hiyo inatokana na kesi namba 19 ya 2021 iliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Joran Bashange.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wabunge waliopita bila kupingwa wako 28.

Kossata ametoa kauli hiyo leo Aprili 5, 2023 kauli alipokuwa akichangia mada katika mjadala wa Twitter Space, unaoendeshwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd uliobeba mada “Zuio la wabunge kupita bila kupingwa litachagiza uwezo wa uchaguzi huru 2025?”

Katika mchango wake, Kossata amesema baada ya hukumu, kinachopaswa kufanya ni wabunge wote 28 waliopita kupitia sheria hiyo kuvuliwa ubunge wao kuanzia siku ambayo sheria hiyo ilitangazwa katika gazeti la serikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Mawaziri ambao wamewahi kutunga sheria ndogondogo itabidi zivunjwe maana watakuwa wametunga wakiwa batili, kile walichosema bungeni inabidi kifutwe na hata mishahara na posho walizopata inabidi warudishe,’amesema Mwanasheria huyo.

Hoja hiyo pia imeungwa mkono na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo aliyesema kuwa ni lazma watu wasimame pamoja katiba ya nchi.

“Huu ni uamuzi ambao Serikali inapaswa kuutumia kama supporting judgment (hukumu saidizi) kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa. Sitarajii kuona Serikali ikikata rufaa dhidi ya uamuzi huu,” amesema Nondo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad