Mwenyekiti wa CCM ajinyonga kisa Milioni 118, ‘Ameacha Ujumbe kwa Familia imsamehe’



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Meshack Mwambogolo amekutwa amejinyonga katika msitu uliopo kitongoji cha Iyenga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali baada ya Rafiki yake aitwaye Joseph Muhume ambaye wanafanya nae biashara pamoja kutoroka na Tsh. Milioni 118.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema mwili wake umekutwa ukiwa umening’inia kwenye mti leo Aprili 24, 2023 asubuhi ambapo alijinyonga kwa kamba ya manila huku akiacha ujumbe kuwa Familia yake imsamehe kwa maamuzi aliyofanya.

Kamanda amesema jana Mwambogolo alitoa Tsh. Milioni 118 na kuziweka kwenye akaunti ya Joseph Muhume kwa ajili ya kununulia kahawa ambapo baada ya kumuingiza fedha hizo Joseph alitoroka.

“Baada ya Mwambogolo kupewa taarifa kuwa Joseph ametoroka alichukua kamba na chupa ya sumu ya kuulia wadudu na kutoweka ndipo mwili wake ulikutwa asubuhi ukiwa unaning’inia kwenye mti huku akiwa ameacha ujumbe ambao unaiomba Familia yake imsamehe kwa uamuzi alioufanya wa kujinyonga”



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad