Nabi 'Hakuna Anayeweza Kunipangia Kikosi Changu...Mashabiki Tulieni'

 


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohammed Nabi amewataka mashabiki wa soka nchini kuacha tabia ya kuwapangia vikosi makocha wao kwa ajili ya mchezo husika kwani kocha ndiyo anajua mfumo atakaotumia na aina ya wachezaji anaowatumia kutokana na mahitaji ya mechi husika.

Nabi amesema hayo leo Jumamosi, Aprili 29, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa marudiano wa robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

“Nitakachokifanya huwa kinafanywa na makocha wengine duniani, sababu kubadilisha timu ni jambo la kawaida sana kwenye soka la kisasa.

“Kocha anabadilisha wachezaji kutokana na mechi ambayo iko mbele yake, ataangalia mfumo anaoenda kucheza na aina ya

wachezaji anaowahitaji kwenye mfumo huo, lazima kuna mabadiliko ambayo nitafanya.

“Sio lazima ambao mashabiki wamezoea kuwasikia kwenye masikio yao, wachezaji nitakaopanga ni wale wanaoendana na mfumo nitakaoutumia kesho.

“Pia, nitaangalia kujituma kwao kwenye mazoezi ambapo najua huyu ameshuka ama yuko vizuri kuingia kwenye mfumo wangu naanaweza kutusaidia kwenye mechi ya kesho.

“Wachezaji nao ni binadamu, wapo wengine ambao ni miaka miwili sasa kila mechi wanacheza, lazima na wao miili ipumzike, sababu kucheza sana mwili wake unaweza kuchoka akashuka kiwango.

“Mwingine anaweza kukaa benchi akiingia akakupa matokeo kuliko hata waliokuwa uwanjani. Kwa hiyo nitaangalia zaidi mfumo wangu ili kupanga kikosi changu.

“Mashabiki tuache mambo ya kizamani kupangiana wachezaji lazima flani acheze, flani asicheze. Hata Ulaya kocha anakuwa na kikosi kipana na anabadilisha kulingana na mahitaji ya siku husika,” amesema Nabi.

Yanga wakiwa na mtaji wa bao 2-0, kesho watashuka katika dimba la Mkapa kukipiga na Rivers United wakisaka tiketi ya kusonga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad