NEMC Walikana Gari Lililotelekezwa Maeneo ya Kisutu


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa taarifa kuhusu video inayotembea kwenye mitandao ya kijamii pamoja na makundi ya whatsApp ikionesha gari lenye kava ya tairi yenye nembo ya NEMC (Wheel cover) limeegeshwa eneo lisilo rasmi likipatiwa huduma.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka imesema “Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linapenda kuutarifu Umma kuwa gari linaloonekana katika video hiyo haina uhusiano wowote na NEMC”

“NEMC inatumia njia mbalimbali katika kujitangaza ikiwemo kuandaa na kusambaza kava za matairi (wheel covers) zenye jumbe wa mazingira kwa wadau wake, magari yote ya NEMC yana namba za usajili na hufanyiwa matengenezo (service) katika gereji iliyoingia Mkataba wa kisheria wa kutoa huduma husika”

“Kwa mantiki hiyo kuonekana kwa gari hilo lenye kava ya tairi lenye nembo ya NEMC haimanishi kuwa gari hilo linamilikiwa na Baraza, hivyo NEMC inawasihi Wananchi video hiyo iliyoleta taharuki na kuchafua Taasisi ya Serikali”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad