Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya leo kwa saa za Marekani.
Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha Kaka yake.
“Nimepewa taarifa na Shemeji (Mke wa Wakili Mkono) kwamba Mzee amefariki nimempigia Shemeji alikuwa analia tu ameshindwa kuongea vizuri, Mzee aliondoka Tanzania tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea”
“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye” #MillardAyoUPDATES #SafiriSALAMA #NimrodMkono 🙏🏿