Ripoti zilizuka Jana Ijumaa kwamba mchezaji huyo kuachana na mke wake, ambaye katika mchakato wa talaka, alidai zaidi ya nusu ya mali ya nyota huyo wa PSG.
Taarifa ya mahakama ilisema Mmorocco huyo hakuwa na mali na alikuwa ameweka mali yake yote, nguo, nyumba, magari, vito vya thamani, na vingine, chini ya jina la mama yake.
Okoye, aliandika kupitia twitter, alihoji kwa nini wanaume wengi wanafurahia kitendo cha Hakimi kuandika Mali zake zote kwa jina la mama yake?
Aliandika, “#JustMyOwnViewAndOpinion Sielewi kwa nini wanaume wengi wanashangilia hadithi hii ya Hakimi? Kama sielewi🤷🏾♂️ Ukweli ni mchungu lakini unahitaji kusemwa. Ikiwa haumwamini, basi usioe rahisi kama hivyo. Au unategemea mkeo ateseke baada ya kuachana?🤷🏾♂️ “Kumbuka!!!Uliyemwamini kwenye mali yako yote na kuandika jina la Mama yako alikuwa mke wa baba yako".
"Mama ambaye ni mama yako alikuwa/pia ni mke wa mtu wakati fulani, kabla hajawa mama yako. Je, kama angefanyiwa hivyohivyo?📌Pls Muoe Mama yako! EOS. #Talaka ya Hakimi.