Limefufuka! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Rayvanny kumuibua mzazi mwenziye kwenye ukurasa wake na kuposti video zinazomuonesha akiwa kwenye pozi la mahaba.
Japo wawili hao hawajaonesha kwamba wawerudiana lakini inaonekana wazi, kuna mahaba kati yao na huwenda mwamba akawa amerudisha majeshi mazima licha ya kuwa wameonekana kwenye video mpya ya Rayvanny, Forever.
Kwenye video hiyo ambayo tayari imetazamwa na watu milioni 1 ikiwa na siku mbili, Fahyma ameigiza kama video queen lakini pia wawili hao kwa sasa wanaposti posti mbalimbali Instagram kuashiria kwamba mambo yamerudi kama zamani.
Rayvanny na Fahyma walibahatika kupata kupata mtoto miaka kadhaa iliyopita wakiwa kwenye mahaba lakini hata hivyo waliachana na baadaye Rayvanny akaingia kwenye penzi na Paula lakini naye baadaye wakaachana na sasa mwamba karudisha majeshi kwa mzazi mwenziye.