Polisi watoa tahadhari kuelekea sikukuu ya Pasaka

Jeshi la Polisi nchini litaendelea kushirikiana na wananchi na waumini wa dini zote  katika kuimarisha  usalama  wa maisha na mali  ikiwemo kubaini na kutanzua uhalifu wa kijinai pamoja na ajali za barabarani  katika kuelekea ibada  za sherehe za sikukuu  ya Pasaka

Hayo yalisemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime makao makuu ya Polisi jijini Dodoma alipokuwa  akitoa taarifa kwa vyombo habari kuhusu tahadhari kuelekea sikukuu ya Pasaka.

Misime alisema kuwa jeshi la polisi nchini katika mikoa na vikosi vyote limejipanga kikamilifu katika kuimarisha doria maeneo ya ibada na kwenye viwanja vya starehe  kuhakikisha kwamba sherehe hizo zinasherekewa kwa amani na utulivu. 

“Jambo kubwa ni kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake katika kuimarisha usalama wa raia na mali.” alisema Misime.

Aidha,  alitoa rai kwa viongozi wa nyumba za ibada ambazo zitakuwa na ratiba za ibada kuimarisha kamati za ulinzi  na kuwasiliana  na wakuu wa polisi wa maeneo yao ili waweze kujadili namna ya kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa ibada hizo. 

Vilevile amewataka Wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao kwa kuangalia na kutambua maeneo yote watakayokuwa wanasheherekea 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad