Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amedai hakuna #Uwajibikaji wa kutosha kutokana na mwendelezo wa ripoti zinazotolewa na idara hiyo kila Mwaka
Amesema “Mfano Ripoti ya Mwaka 2022 inaeleza kulikuwa na mapendekezo 205 yaliyotolewa Mwaka 2020, kati ya hayo 60% yamejibiwa, 40% hayakujibiwa. Inamaanisha kulikuwa na mapendekezo 82 hayakujibiwa na hatupewi taarifa yaliishiaje.”
Ameongeza “Mfano suala la kusema ‘Linaendelea kutekelezwa’ lina ukakasi, Ripoti inapotoka kunakuwa na Miaka miwili nyuma ya ukaguzi, hivyo jumla kunakuwa kama kuna Miaka mitatu hapo kati, sasa inakuwaje jambo linaendelea kutekelezwa kwa Miaka mitatu?”