Rais Samia Awateua Diamond Platnumz na Shilole

 


 Rais Samia Awateua Diamond Platnumz na Shilole 

Mapema leo Aprili 25, 2023, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani Kitaifa ametangaza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amewateua wasanii na Wafanyabiashara Diamond Platnumz na Shilole kuwa wajumbe na Mabalozi wa Kupambana na Ugonjwa wa Malaria.


Waziri Ummy amesema, anaamini wasanii hao wana idadi kubwa ya wafuasi kwenye mitandao yao ya kijamii hususan Instagram, watakapoweka jambo lolote kuhusu suala la kujikinga na Malaria basi ndani ya muda mfupi, itawafikia watu wengi.


"Diamond ana wafuasi karibu Milioni 16 hivyo wakiweka posti yao kuhusu Malaria, ndani ya muda huohuo, idadi ya watu wake watakuwa wamepata ujumbe," alisema Ummy.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad