Baada ya kumtumia mama wa mtoto wake kama 'Video Vixen' na kupendezesha video ya wimbo wake wa #Forever @rayvanny amenogewa na mafanikio aliyoyapata kwenye video hiyo na ameahidi kumtumia @fahyvanny kwenye video ya wimbo wake mwingine kwasababu ya uzuri wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye Instastory @rayvanny ameandika "Kwa jinsi alivyo mzuri nashoot nae my next video tena Forever haitoshi". Ikumbukwe video ya wimbo wa Forever ilipata watazamaji 'Views" Milioni 1 ndani ya siku moja jambo ambalo linatajwa kuwa @fahyvanny ndio sababu kubwa kutokana na uwepo wake kwenye video hiyo.