Waswahili wanasema Kisiki cha Mpingo ni kigumu kuking’oa kuliko aina nyingine ya mti.
Tunaweza kusema @simbasctanzania wamekutana na ‘Kisiki cha Mpingo’ hatua ya robo fainali ya Champions League.
Huo ndiyo ukomavu wenyewe, kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa hasa hatua ya robo fainali hutarajii kukutana na timu nyepesi.
Waydad Casablanca hawa ndiyo Mabingwa watetezi wa Kombe hili la CAF Champions League.
Waydad ni mara moja tu ndani ya miaka sita (6) ndiyo hawakuvuka hatua hii ya Robo Fainali ya CAFCL.
Ndani ya miaka sita (6), Waydad wamefika Fainali mara tatu na katika hizo 3 wamefanikiwa kuchukua Ubingwa mara mbili.
‘Simple’ tunaweza kusema Mnyama amekutana na ‘Kisiki cha Mpingo’ haking’oleki kwa Panga wala Shoka unahitaji Greda.
=> 2022/23 Bingwa Mtetezi
=> 2021 Nusu Fainali
=> 2020 Nusu Fainali
=> 2019 Washindi wa Pili
=> 2018 Robo Fainali
=> 2017 Mabingwa
Imeandikwa na @fumo255