Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya kibiashara ili kuhakikisha biashara kati ya nchi hizo zinaimarika.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 27, 2023, mara baada ya Rais Kagame kuwasili na kufanya naye mazungumzo maalum ikiwa ni ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
"Tumeiona haja ya kukuza biashara na kuweka miundombinu ya kukuza biashara kwa sababu kiwango cha biashara tulichonacho hakiendani na rasilimali tulizonazo kwa nchi mbili na uhusiano mzuri uliopo na tumemhakikishia kwamba Tanzania sasa tunaimarisha bandari zetu," amesema Rais Samia
Kuhusu masuala ya usalama Rais Samia amesema, "Tumezungumza masuala ya ulinzi na usalama na tukakubaliana kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viendelee kufanya kazi kwa pamoja ili tuhakikishe usalama kwenye nchi zetu na ukanda wa Afrika Mashariki".
Kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema, "Amani na utulivu hitaji muhimu sana kwa ajili ya amendeleo na umoja wa Afrika na Mh Rais Samia kwa mara nyingine tena ninakushukuru kwa mapokezi mazuri yanayotuifanya tujisikie tuko nyumbani,".