Saba washikiliwa na Polisi kwa mauaji, ufukuaji makaburi



Kufuatia kusambaa kwa taarifa ya kufukuliwa kaburi la mzee mmoja huko Wilayani Manyoni na kudaiwa kuchukuliwa baadhi ya viungo, huku watuhumiwa saba waliofanya mauaji na kufukuwa makaburi wakishikiliwa na Jeshi la Polisi ambalo pia limeitaka jamii kuondokana na fikra potofu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime imeeleza kuwa uchunguzi umebaini kuwa kilichochukuliwa katika kaburi lililofukuliwa hivi karibuni na wahalifu ni nguo, cheni, saa, pete na viatu vya marehemu na hakuna kiungo kilichoondolewa.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “matukio haya ya kishirikina huko wilayani Manyoni kwa uchunguzi uliofanyika, umebaini yanaongozwa na imani potofu za kishirikina ambazo ni aibu na pia ni uhalifu.

Tangu matukio haya yaanze kutokea wilayani humo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limewakamata watuhumiwa saba waliofanya mauaji na kufukuwa makaburi.”

Misime ameongeza kuwa,

 “Watuhumiwa hao saba walifikishwa mahakamani tarehe 04.04.2023. mtandao huo wa watu wenye imani hizo potofu za kuua na kufukua makaburi kwa lengo la kupata viungo na mali nyingine za marehemu unaonesha bado upo wengine na Jeshi la Polisi muda si mrefu litaumaliza na wahusika watafikishwa mahakamani.”

Aidha, Jeshi la Polisi limesema pamoja na jitihada zinafanywa za kukamata wahalifu hao na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na fikra hizo potofu, wananchi wanatakiwa kukubali kubadilika na kuachana na imani hizo mbaya kwani ni kosa la jinai kufukuwa makaburi na ni aibu kwa dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia kuendekeza imani hizo potofu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad