Sakata la Fei Toto kama la Msuva, TFF kuvunja mkataba mmmh! - Jasmine

 


Msimamizi wa mchezaji Feisal Salum katika sakata lake na Yanga, Jasmine Razack amesema kuwa Kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zinaruhusu pande zilizoingia mkataba (klabu na mchezaji) kuvunja mkataba huo na si mtu wa tatu (Shirikisho la Soka la nchi husika).


Jasmine amedai kuwa kanuni hiyo ameikuta Tanzania pekee ambapo TFF ina mamlaka ya kuvunja mkataba wa mchezaji na klabu jambo ambalo FIFA halipo.


Aidha, ameongeza kuwa Simon Msuva wakati anavunja mkataba na Wydad Casablanca aliiandikia barua klabu yake hiyo moja kwa moja.


“Msuva alipokuwa Morocco [Wydad Casablanca] alipotaka kuvunja mkataba, hakupitia chama cha soka cha Morocco. Aliandika barua moja kwa moja kwa klabu, hii ni sheria ambayo pia FIFA wanaitambua, heiwezekani ‘third part’ kuvunja mkabata.


“Lakini Tanzania nimekutana na hiki kipengele kwenye kanuni za TFF [kanuni ya 74.14] kwamba, endapo kuna mgogoro baina ya klabu na mchezaji chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba ni Kamati ya Hadhi za Wachezaji.


“Nilishangaa sana kwa sababu ni kitu ambacho kinakinzana na sheria za FIFA! Haiwezekani ‘third part’ ambayo si sehemu ya mkataba yenyewe ndio iwe na mamlaka ya kuvunja mkataba.


“Nikaenda mbali zaidi kutaka kujua kwa nini hii kanuni imewekwa? Nikaambiwa imewekwa kwa ajili ya kulinda wachezaji na klabu. Zamani wachezaji walikuwa wanafukuzwa kiholela kwenye klabu zao na wachezaji walikuwa wanajiondokea.


“Kwa hiyo vipengele hivyo viliwekwa kudhibiti kuachana kienyeji. Nikaona ni sawa. Lakini ni rahisi kwa klabu kumuacha mchezaji kwa sababu inakuwa ipo kwenye kipengele cha mkataba," amesema Jasmine.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad