Sakata la Ujauzito wa Masha LOVE Kutoonekana Mwenye Afunguka "Ujauzito Wangu Umekimbilia Kwenye Mbavu"



Mrembo wa mjini asiyeishiwa vituko mjini, Masha Love ametoa kali nyingine kwa kudai ujauzito wake umekimbilia kwenye mbavu ndio maana watu wanashindwa kuona tumbo lake lilikua.


Masha ameyasema hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano na Diva wa Wasafi Fm ambapo alipoulizwa kuhusu ujauzito huo anaodai ni wa muigizaji Jimmy Mafufu, ndipo alipojibu inshu hiyo.


"Unajua Diva wewe ni mwanamke kama unavyojua haya mashaka ya mimba kuna wengine zinakimbilia kwenye maziwa wengine kwenye mbavu hivyo watu wasubiri tu wataona nikijifungua," alisema Masha.


Masha alimaliza kwa kusema, yeye kwa sasa hawako sawa na baba kijacho wake na aliyempa nafasi kwa sasa katika mahusiano ni aliyekuwa x wake, Dr Kumbuka ambaye naye huwa anamkwaza lakini hana jinsi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad