Sakata mmomonyoko wa maadili na linalosababisha kuongezeka kwa wimbi la watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na mapenzi kinyume cha maumbile (ushoga) limechuykua sura mpya baada ya wabunge kuchachamaa wakiitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kulinusutu Taifa.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, Aprili 11, 2023 na Mbunge Jimbo la Makete, Festo Sanga wakati akichangia hoja Bungeni.
“Suala la maadili namalezi, haya ni mambo makubwa yanayotikisa taifa hili kwa sasa. Kama suala la mapenzi ya jinsia moja hatutalipigia kelele sisi wabunge hapa, nina uhakika miaka 30, au 40 ama 50 tutakuwa na viongozi wanaojihusisha na mambo haya.
“Ubunge wetu ni kwa ajili ya wananchi walioko kule mtaani na haya yanayofanyika wanayaona na sisi tupo kimya. Huu sio utamaduni wetu Waafrika, vitabu vya dini vinakataza, tukijidai kama sisi ni vipofu kana kwamba hatuoni haya yanayoendelea, miaka 30 ijayo nusu ya Bunge wanaweza kuwa ni mashoga wamekaa humu ndani.
“Leo tunajenga SGR, tunajenga Viwanja vya Ndege, tunawekeza kwa kutumia pesa nyingi, tunajenga kwa ajili ya kizazi kipi? Lazima tuanze sasa ili tulinde kizazi chetu. Kwa sababu ya misaada tuwe tayari kuachia kizazi chetu kingie kwenye damu ya Sodoma na Gomola? Hiyo haiwezekani.
“Kama makanisa, misikiti, Bunge havitasimama, kuna siku yataongozwa na watu waliosimama katika upande huo. Ninaomba tuchukue tahadhari na tufanye maamuzi sasa, adui ameonyesha mlango aliyopo na sisi tuonyeshe silaha tulizo nazo,” amesema Sanga.