Serikali: Hakuna Mtanzania Aliyeumia Mapigano Sudan

Tanzania imeungana na nchi wanachama na wajumbe wa Amani barani Afrika kulaani mapigano yanayoendelea Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum kati ya Jeshi la Serikali na kundi la wanamgambo la RSF.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax ameliambia Bunge kuwa hakuna Mtanzania aliyeathirika na mapigano hayo hata hivyo Tanzania imeyataka makundi hasimu kusitisha mapigano mara moja.

Watu 185 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 1000 kujeruhiwa kutokana na mapigano hayo yaliyoanza Aprili 15, 2023 na kudhorotesha jitihada za kutafuta amani nchini humo.

Nchini Sudan kuna watanzania wapatao 210 ambapo 171 ni Wanafunzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad