Shambulio la kujitoa mhanga laua na kujeruhi zaidi ya watu 70 Mali.




Watu wasiopungua 10 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika shambulio la bomu karibu na kambi ya kijeshi na uwanja wa ndege katikati mwa Mali.

Yacouba Maiga, msemaji wa Gavana wa mkoa wa Mopti amesema, zaidi ya watu 60 walijeruhiwa pia katika shambulio hilo lililotokea kwenye mji wa Sevare ulioko katika mkoa huo mapema jana.

Kwa mujibu wa Maiga, mripuko huo uliharibu takribani nyumba 20 katika mji huo. Ameongeza kuwa, kuna jumla ya watu tisa waliofariki na takriban 60 wamejeruhiwa, wote wakiwa raia.

Kanali Souleymane Dembele, msemaji wa jeshi la Mali, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba takriban watu 10 waliuawa katika hujuma hiyo.

Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na serikali ya Bamako, jana hiyohiyo Jeshi la Mali liliteketeza ngome ya magaidi huko Mourdiah na kuwaangamiza magaidi 60 katika mji wa Boni, ambao nao pia uko katika mkoa wa Mopti.

Tangu mwaka 2012, Mali imekabiliwa na machafuko kufuatia kuenea kwa makundi yenye misimamo ya kufurutu mpaka nchini humo.

Hakukuwa na yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo mpaka sasa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad