Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi maalum ya kuwapa ushindi.
UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, wachezaji wao wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 16, huku wakifanya mazoezi maalum ya kuwapa ushindi.
Miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao hawakuwa fiti hivi karibuni ni Shomari Kapombe aliyepata maumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca, Aishi Manula na Henock Inonga walipata maumivu katika mchezo dhidi ya Ihefu ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, alisema: “Baada ya kukamilisha mchezo wetu dhidi ya Ihefu ugenini, kikosi kimerejea jana (juzi) na wachezaji leo (jana) wamewasili kambini na jioni wataanza mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga.
“Wachezaji wote wapo vizuri, hakuna majeruhi, kwa wale ambao walipata majeraha maendeleo yao ni mazuri,” alisema Ally.
STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA