Simba yaifuata Azam nusu fainali



PAMBANO la robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Simba na Ihefu FC limemalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es salaam kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 na kuifuata Azam Fc kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.

Ilikuwa siku nzuri kazini kwa straika Jean Baleke akitupia mabao matatu (hat trick), huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na Said Ntibazonkiza na Pape Ousmane Sakho aliyeingia kutoka benchi.

Baleke amefikisha mabao 12 kwenye mashindano yote na manne ya ASFC, mbali na matano ya Ligi Kuu na mengine matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bao la kufutia machozi la  Ihefu lilifungwa na kiungo Raphael Daud dakika ya 61 akiunganisha kwa kichwa mpira wa friikikii uliopigwa na Never Tigere.
Ushindi wa Simba unaipa nafasi ya kucheza nusu fainali dhidi ya Azam iliyoitoa Mtibwa Sugar kwa kuichapa mabao 2-0 mapema wiki hii.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad