Simba, Yanga zapanda viwango CAF





Klabu za Simba na Yanga zimepanda katika viwango vya ubora kwenye michuano ya CAF baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho


Klabu ya Simba imepanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 11 mpaka nafasi ya 7

Simba ni miongoni mwa timu nane zilizofuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa wakisubiri droo ya mechi za robo fainali itakayopigwa Jumatano huko Misri

Yanga imepanda kwa nafasi 26 kutoka nafasi ya 46 mpaka nafasi ya 20 baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho

Kwa mara ya kwanza Yanga imeingia katika klabu 20 bora barani Afrika

Wananchi wanaweza kusogea juu zaidi kama watafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad