Steve Nyerere: Atakayekuja Kwenye Jeneza Langu Nitamnasa Kibao

 


Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere amewataka watu kusaidiana wakati wamatatizo huku akidai siku akifa, atafufuka kwenye jeneza na kumnasa kibao mtu mnafiki ambaye amekuja kumuaga.

Steve amedai kuwa, hakuna sababu ya kwenda kuuaga mwili wake akiwa amefariki wakati kipindi alipokuwa hai walishindwa kumsaidia.

Ameyasema hayo juzi Jumanne wakati ya mkutano wa waandishi wa Habari Serena Hotel Dar ss Salaam akimtambulisha kwenye muziki mwanadada Jack ambaye ni mlemavu wa uti wa mgongo.

Katika hatua nyingine, supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz alimsaidia msanii huyo ili aweze atimize malengo yake na kuahidi kumsaidia kuandaa kazi zake pamoja kiti cha umeme cha kutembelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad