Taarifa Kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Kuhusu Utapeli


Taarifa kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imetoa tahadhali kutokana na kuwepo na baadhi ya watu wanaotumia jina la Ofisi ya kurugenzi wa Mawasiliano
ya Rais Ikulu kwa kutumia jina la Zuhura Yunus @venusnyotah kwa barua pepe zuhurayunus250@gmail.com na kuwatapeli watu kuwa wanaweza kuwaunganisha na kupata Teuzi mbalimbali na nafasi za kazi.

Aidha Watu hao kupitia barua pepe hiyo wamekua wakiombwa kutuma kiasi cha fedha ili wapate nafasi za Teuzi katika taasisi mbalimbali serikalini.

kutokana na hayo kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeweka wazi kuwa haihusiki na barua pepe hiyo na maamuzi yeyote ya Uteuzi. Hivyo kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imetoa tahadhali watu waepuke kutapeliwa pindi tu wanapo pokea taarifa za namna hiyo.
-
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad