Tariq Aliyemwagiwa Tindikali Asimulia Chanzo 'Mtuhumiwa Alinitaka Kimapenzi



Jamaa ambaye alimwagiwa tindikali mwaka jana, Tariq Kipemba kwa mara ya kwanza amesimulia kwa undani tukio hilo lililotokea katika aneo alilokuwa anaishi, Moshi mkoani Kilimanjaro.


Alianza kwa kusema, tukio hilo lilimsibu baada ya kukutana na jamaa ambaye alihamia kwenye eneo walilokuwa wanaishi wapangaji tofauti wakiwa ni mabachela.


"Hiyo nyumba tulikuwa tunaishi mabachela na tulikuwa tunafahamiana. Sasa alihamia huyu jamaa ambaye alikuwa mgeni, tukazoeana akawa rafiki yangu tukawa tunatoka naye viwanja kwa kuwa mimi wakati huo sikuwa na kazi zangu. Mimi nafanya kazi za utalii," anasema Tariq.


Akizidi kusimulia, Tariq alisema, jamaa huyo alimuelezea kwamba ana jamaa zake Ujerumani na baadaye walikuja kukutana na jamaa wake mwingine ambaye naye alikuwa anaishi Ujerumani hivyo wakawa marafiki watatu pamoja.


"Tulikuwa tunatoka wote na kuwarudisha maana mimi nilikuwa situmii kilevi sasa wakati wao wakitumia kilevi mimi ndio nilikuwa dereva wao nawarudisha nyumbani," anasema Tariq.


Anasema ghafla jamaa huyo alianza kumtumia meseji ambazo alikuwa hazielewi na alipokuwa anamuuliza asubuhi alikuwa anasema ni ulevi hivyo aachane nazo.


"Meseji anakuambia anaomba kulala na wewe mimi nikawa simjibu na kuna siku aliniambia kwamba amenimisi na nini, nilishangaa kwa mwanaume kummisi mwanaume mwenzake," anasema.


Alisema kuna siku alivunja ukimya na kumtongoza kabisa na ndipo Tariq akapunguza mazoea naye.


"Alipoona mimi sielekei akahamia kwa jamaa yetu alikuwa anasoma akaanza kumtongoza ikashindikana na wote tukawa tushamjua, baadaye akanirudia tena mimi na kuniambia anataka kunipa pesa alizoahidi kunikopesha tena safari hii akasema anataka kunipa bure ila kwa sharti la kwamba nilale naye," anasema.


Tariq anasema alimkatalia na ndipo ukawa ugomvi kati yake hadi kujikuta amefanyiwa tukio hilo la kikatili na kumwagiwa tindikali.


"Kabla ya tukio zilikuja bodaboda nyingi pale nyumbani, wakawa wanakula wanakunywa kwa yule jamaa, siku ya Jummaosi ambayo mimi ndio nilipata tatizo nilikuwa nimekaa kwenye restaurant, wakaja washkaji zangu tukaa akiwemo yule rasta ambaye alikuwa anafahamiana na yule jamaa ambaye alikuwa mtuhumiwa," anasema.


Anasema baada ya muda aliwaaga washkaji zake hao kwamba anakwenda nyumbani mara moja kuchukua koti ndipo akiwa njiani walipotokea vijana wawili wakiwa kwenye bodaboda.


Anasema walipompita, mmoja aliyekuwa nyuma alishtuka kama kumuona na ndipo mmoja wao alipomwagia acid kali usoni na nikapata maumivu makali.


Anasema alipata msaada akakimbizwa Hospitali ya KCMC na kupata msaada, akiwa anaona lakini kesho yake ndio akapoteza nuru akawa haoni.


Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa lakini baadaye aliachiwa wakati yeye akiwa kwenye matibabu nchini India na mpaka leo kesi ni kama imeisha juu kwa juu, hakuna kinachondelea huku mtuhimiwa akitamba mtaani.


Tariq amerejea akiwa anaona kwa kutumia jicho moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad