Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ imesogeza mbele shauri la kiungo Feisal Salum ‘Fei toto’ la kutaka kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga hadi Mei 5 mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa mchezaji, Feisal aliwasilisha ombi la kutaka kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga mwezi uliopita baada ya hapo awali kushindwa shauri la kwanza na shauri la marejeo na kamati hiyo kuamua mchezaji huyo kurejea klabu ya Yanga.
Vuta nikuvute hiyo ilianza disemba mwaka 2022 ambapo aliwasilisha barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo na kuilipa Yanga milioni mia moja kumi na mbili kitendo ambacho klabu yake ya Yanga imekitafsiri kama kukiuka taratibu za kuvunja mkataba