Timu ambazo Yanga atakutana nazo Robo fainali kombe la shirikisho hizi hapa






Baada ya Yanga kuizamisha TP Mazembe kwenye dimba lao la nyumbani huko DR Congo kwa kuwachapa bao 1-0, US Monastir walipaswa kushinda angalau mabao matatu dhidi ya Real Bamako ili kuweza kuiondosha Yanga kileleni mwa kundi D


HAIKUWEZEKANA kwani Monastir walipata ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kuihakikishia Yanga kumaliza kileleni mwa kundi  wakiwa na alama 13

Yanga sasa itakuwa na faida kwenye hatua ya robo fainali kwa kuanzia ugenini na kumalizia mechi ya pili nyumbani

Yanga, AS FAR, Malumo Galants na ASEC Mimosas zimemaliza vinara wa makundi wakati US Monastir, Rivers United, USM Alger na Pyramids zimemaliza katika nafasi ya pili


Katika hatua ya robo fainali Yanga itamenyana na kati ya Rivers United, USM Alger au Pyramids

Droo ya mechi za robo fainali itafanyika siku ya Jumatano


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad