TMA "Mvua ipo Hadi Mwezi wa Sita"

 


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua zinazonyesha kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya nchi zitaendelea mpaka mwezi wa sita mwaka huu na vitakuwa ni vipindi vifupi na virefu vya mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha madhara ikiwemo mafuriko na magonjwa ya milipuko.


Akizungumza na EATV leo Mtaalam na Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA Joyce Makwata, amesema mikoa ambayo itaathirika zaidi na mvua hizo ni Ile ya Dar es Salaam Tanga, Pwani, Morogoro, Visiwa vya Unguja na Mafia.


Amesema licha ya kwamba mvua hizo ni za masika lakini wananchi wanapaswa kuhakikisha kwamba wanafuatilia  kwa karibu taarifa za mamlaka ili kufahamu mwelekeo wa hali ya hewa kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad