Urembo wa Askari Huyu, Wananchi Wapiga Simu 'Fire' Kuomba Namba zake



Nchini Nigeria kuna stori ambayo inatrend sana, na hii inahusiana na huyo mrembo pichani ambaye ni mfanyakazi wa Zimamoto ambaye anaitwa Dooshima Dennis.


Dooshima ni mwanamke mrembo ambaye anafanya kazi kama Afisa wa Jeshi la Zimamoto, kutokana na jinsi alivyo ametokea kuwa maarufu sana na yeye mwenyewe kwenye account yake ya Twitter anajielezea kuwa ni Nigerian first celebrity fight fighter, kwamba ni Afisa wa Zimamoto wa kwanza mwanamke mrembo na maarufu, na umaarufu wake umetokana na jinsi alivyo mrembo.


Kilichotokea ni kwamba watu wengi sana huko Nigeria wamekuwa wakijaribu bahati zao wakimsumbua sana kiasi ambacho imekuwa kero mpaka kwenye hofisi za Jeshi la Zimamoto kwa sababu wanachokifanya ni kwamba wanapiga simu katika Jeshi la Zimamoto wakimuulizia Dooshima.


Kuwa wanataka kuongea nae na wengine wanataka namba yake, umekuwa ni usumbufu ambao umemfanya awaonye watu hao hasa wanaume waache kumsumbua.


Dooshima amewambia wanaume wa Nigeria kwamba wanamuweka katika matatizo, amewaomba wawe siriasi waache kupiga simu kwenye chumba cha Zimamoto kuomba namba yake ya simu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad