Wachezaji Mayele, Baleke; Watafanya Makubwa Sana CAF

 

Wachezaji Mayele, Baleke; Watafanya Makubwa Sana CAF 

Nyota Simba SC Jean Baleke na Fiston Mayele anayekipiga Young Africans, wamepewa nafasi kubwa ya kuzibeba timu zao kufanya vizuri katika michezo wa Mkondo wa Pili ya Robo Fainali ya michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.


Simba SC inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, itashuka dimbani Keshokutwa kuivaa Wydad AC nchini Morocco wakati Young Africans inayoshiriki Kombe la Shirikisho Barani humo itavaana na Rivers United ya Nigeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dár es salaam.


Timu hizo zitaingia dimbani wakati Simba ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Young Africans ikiwa imeshinda mabao 2-0 ugenini dhidi ya Rivers United.


Pamoja na timu hizo kuanza na ushindi, washambuliaji Baleke na Mayele wamekuwa na kasi nzuri ya upachikaji wa mabao katika mashindano hayo.


Katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Baleke ni miongoni mwa washambuliaji waliofunga mabao mengi hadi sasa wakati Mayele ndiye kinara wa waliopachika mabao katika Kombe la Shirikisho Barani humo.


Baleke amefunga mabao manne katika michuano hiyo msimu huu wakati Mayele akiwa amepachika matano.


Baleke amepachika mabao hayo wakati Simba SC ilipovaana na Horoya (2), Raja Casablanca (1) na Wydad AC (1) huku Mayele ya akifunga dhidi ya AS Real Bamako (2), US Monastir (1) na Rivers United (2).


Tuchel avunja ukimya, Sina tatizo na Muller Baadhi makocha wa soka nchini wamewapongeza nyota hao kutoka DR Congo kwa uwezo wa kufumania nyavu na wanaamini wanaweza kuendeleza kuzibeba timu hizo katika michezo ya mwishoni mwa juma hili.


Mchezaji na Kocha wa zamani wa Simba SC, King Abdallah Kibadeni Mputa amesema wachezaji hao wanatambua thamani yao wanapokuwa uwanjani.


Kibadeni amesema anaamini nyota hao wawili wataendelea kuonyesha uwezo wa kufunga mabao katika michezo ya mwishoni mwa juma hili, na kuzisaidia timu zao zinazohitaji ushindi ili zitinge Nusu Fainali katika michuano ya Kimataifa.


“Wachezaji hawa wanatambua kipi wanafanya ndiyo maana wanang’ara katika kila mchezo,” amesema Kibadeni


Naye Kocha timu taifa ya vijana chini ya umri miaka 16, Maalimu Salehe ‘Romario’ amesema utulivu, kujituma na uwezo wa wachezaji hao utazisaidia timu zao kupenya katika hatua Robo Fainali na kutinga Nusu Fainali mwishoni mwa juma hili.


“Mayele na Baleke wanazingatia maelekezo ya makocha wao, ndiyo maana wanafanya vizuri, kitu ambacho baadhi ya wachezaji wetu hapa nchini wanashindwa kufanya,” amesema Salehe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad