Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa idhini ya kurudia Mtihani kwa Wanafunzi 337 waliofutiwa Matokeo ya Kidato cha 4 kwa Mwaka 2022 baada ya kuomba fursa ya Kurudia Mtihani huo
Kati yao, Wanafunzi 4 walifutiwa Matokeo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) baada ya kuandika Matusi katika Mitihani yao
Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda, amesema Utaratibu wa kurudia Mitihani utakwenda sambamba na Mitihani ya Kidato cha 6 ambayo inatarajiwa kuanza Mei 2, 2023. Watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia Mitihani hiyo