Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imefanikiwa kuwaondosha wanafunzi wote wa Kitanzania wanaosoma nchini Sudan.
Safari ya kurejea nyumbani ilianzia Khartoum kwa mabasi, majira ya saa 7.30 mchana ya April 24, 2023 na kuelekea Mji wa Al Qadarif ambao upo takriban kilometa 420 kutoka Khartoum.
Msafara ulifika Al Qadarif usiku na kulazimika kulala kutokana na usalama na kuondoka asubuhi ya tarehe 25 April 2023 kulekea Mji wa Metema, Ethiopia ambao unapakana na Sudan. Metema Iko kilemet 161 kutoka Al Qadarif.
Kutoka Metema, Msafara ulianza safari kuelekea Mji wa Gondar, Ethiopia ambao uko kilometer 220.
Kutoka Gondar Watanzania hao 200 na raia 10 wa nchi nyingine za Afrika walisafiri Kwa ndege kwenda uwanja wa Bole, Addis Ababa.
Kutoka Addis Ababa watachukuliwa na Ndege ya Tanzania (ATCL) dreamliner kuja Dar es Salaam.