Ng Chuan Sing na mkewe, Lim Siew Guan, takriban katika miaka yao ya 80, walinunua samaki aina ya puffer bila kujua kutoka kwa mchuuzi wa mtandaoni huko Johor na wakamla Machi 25 na kulingana arida la PEOPLE, binti yao Ng Ai Lee alisema wazazi wake walinunua samaki mara kwa mara kutoka mchuuzi huyo kwa miaka mingi na aliamini baba yake asingali nunua kitu ambacho kingehatarisha maisha yao.
Baada ya kula samaki hao, Lim alipata shida kupumua na kutetemeka huku mumewe akianza kupata dalili kama hizo saa moja baadaye nipo Walisafirishwa hadi hospitali ya eneo hilo, ambapo Lim alitangazwa kuwa amekufa saa kadhaa baadaye saa 7:00 p.m. Sing nae akafariki siku ya Jumamosi.
“Wale waliohusika na vifo vyao wanapaswa kuwajibika pia ninatumai serikali ya Malaysia itaimarisha utekelezaji na kusaidia kuongeza uelewa wa umma juu ya sumu ya pufferfish ili kuzuia matukio kama haya kutokea tena,” Lee alisema.
Samaki Pufferfish ambe pia anajulikana kama fugu, ni moja ya chakula kitamu huko Japani, lakini pia hutumiwa katika nchi zingine, pamoja na Malaysia. Nchini Malaysia, samaki aina ya pufferfish mara nyingi hutumika kwa kuwekwa kwenye sehemu ya sahani inayoitwa “Yee Sang,” sahani ya kitamaduni inayoliwa wakati wa sherehe za Mwaka Mpya wa Kichina.
Ini, ovari na ngozi, miongoni mwa sehemu nyingine katika samaki huyo wa Kijapani aina puffer zinaweza kuwa na hatari ya kiasi cha tetrodotoxin, aina ya neurotoxin yaani samaki huyu ana sumu mara mia kutofautisha sehemu nyingine kadhaa za samaki huyo zenye sumu ya kutosha kusababisha kifo cha cha ghafla wani takati wakumtengeneza samaki huyu uangalifu mkubwa lazima uchukuliwe ili kuhakikisha kwamba sehemu hizi zimeondolewa vya kutosha na kwamba hazichafui nyama/minofu ya samaki huyu.
Nchini kote, kuna takriban kesi 20-40 za sumu ya fugu kwa mwaka, na kati ya vifo 0-3. Vifo vingi hutokea kama matokeo ya watu kukamata na kujaribu kuandaa samaki wenyewe au wakati wa kula wamedai kupewa ini yenye sumu.
Dalili za kula samaki aina ya pufferfish/fugu ni pamoja na kuwashwa kwa midomo na kizunguzungu kulingana na CNN, dalili zinaweza kuanza dakika 20 baada ya kula samaki hata hivyo, kuuza bidhaa zenye sumu si lazima kuwa kinyume cha sheria nchini Malaysia lakini kunadhibitiwa sana.
Nchini Malaysia, uagizaji, uuzaji na utumiaji wa samaki aina ya pufferfish unakabiliwa na leseni kali na udhibiti wa serikali.
Nchini Malaysia, wapishi walio na leseni na waliofunzwa pekee ndio wanaoruhusiwa kutayarisha na kuhudumia samaki aina ya pufferfish/fugu na lazima wafuate miongozo madhubuti ili kuhakikisha kuwa samaki ni salama kwa matumizi zaidi ya hayo, uagizaji wa samaki aina ya pufferfish unadhibitiwa sana ili kuhakikisha kuwa samaki walio salama na waliotayarishwa ipasavyo pekee ndio wanaouzwa nchini.