Watoto 37 Wamepoteza Maisha Katika Matukio ya Kusombwa na maji



Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime

JESHI la Jeshi la Polisi Tanzania limetanga kuwa watoto 37 wamepoteza maisha katika matukio ya kusombwa na maji katika maeneo mbalimbali nchini kati ya mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu. Anaripoti Abel Paul wa Jeshi la Polisi, Dar es Salaam … (endelea).

Pia Jeshi hilo linapenda tahadhari kwa wananchi wanatumia vibaya mitaandao ya kijamii hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendela kunyesha kutoa taarifa mbalimbali ambazo siyo rasmi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema matukio ya vifo vya watoto hao ambavyo vimetokena na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yametokea katika baadhi ya mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Katavi, Kilimanjaro, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Pwani na Rukwa.

Misime amebainisha kuwa matukio hayo kuna baadhi ya wazazi wanashindwa kuwalinda watoto wao ambapo amesema Jeshi hilo litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kushindwa kutekeleza wajibu wa kisheria na kusababisha mtoto kupata madhara.

Sambamba na hilo amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini lingependa kutoa tahadhari na onyo kwa wale wachache wanaoendelea kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kusababisha hofu, taharuki kwa wananchi.

Pia amesema kuwa kuna taarifa imerushwa hivi majuzi ikionyesha gari aina ya Toyota Land Cruiser hardtop ikisombwa maji ambapo mhalifu aliyetengeneza uongo huo aliandika tukio hilo limetokea muda mfupi huko Arusha, ambapo usahihi tukio hilo lilitokea mwaka jana nchini Sudan Kusini.

Aidha Misime amesema jamii iendelee kuwakumbusha watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya binadamu wenzao wana magonjwa na wanapopata taarifa za kushtua kama hizo wanaweza kupata madhara makubwa zaidi hata kupoteza maisha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad