Mexico. Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya puto ya hewa moto ‘Hot Air Balloon’ waliyokuwa wamepanda kuwaka moto katika mji wa Mexico.
Balloon hio ilikuwa ikiruka karibu na eneo maarufu la kiutalii la Teotihuacan ilishika moto siku ya Jumamosi Aprili 1, huku chanzo kikiwa bado hakijulikani.
Maafisa katika jimbo la Mexico, ambalo linapakana na mji mkuu, walisema waliofariki ni mwanamke mwenye umri wa miaka 39 na mwanaume mwenye umri wa miaka 50, ambao majina yao hayajafahamika na majeruhi ni msichana mdogo aliyeungua na kuvunjika mkono.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Washington Post limeripoti kuwa ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la magofu la kabla ya Uhispania la Teotihuacan, kaskazini mwa Mexico City, ambalo ni eneo maarufu kwa watalii wanaopanda puto.
Kulingana na video ya tukio hilo iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, waliokuwa ndani ya puto hilo walionekana kuanguka kutoka juu, Polisi wa eneo hilo wanaendelea na uchunguzi.
Imeandaliwa na Sute Kamwelwe