"Tunaitaka DART kuingia mkataba mara moja na TPDC na kubadilisha mabasi ya mwendokasi kutoka kutumia dizeli, kwenda kutumia gesi asilia."
Amesema Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi wa chama cha ACT Wazalendo, Emanuel Mvula na kuongeza kuwa hilo litapunguza uzalishaji wa hewa ukaa, litaokoa mamilioni ya fedha zinazotumika kuagiza mafuta nje, gharama za uendeshaji zitashuka na nauli zitashuka.