Waziri wa Afya Apendekeza Hospitali ya Mirembe Ibadilishwe Jina


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amependekeza kubadilishwa kwa jina la Hospitali ya Mirembe ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kupata matibu kwenye hospitali hiyo.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Ushauri katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Waziri Ummy ameshauri kwamba hospitali hiyo iitwe Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili ambapo ameisisitizia bodi hiyo kujikita katika kukuza afya ya akili ambayo ni lengo kuu la kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

Hospitali ya Mirembe imekuwa ikijihusisha na huduma za tiba ya akili, tafiti mbalimbali za maradhi yatokanayo na afya ya akili, mafunzo ya afya ya akili na uhamasishaji kwa jamii juu ya uelewa wa afya ya akili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad