Akiwasilisha Uchambuzi wa #RipotiYaCAG, Kiongozi wa Chama hicho, #ZittoKabwe amesema Ripoti imeibua hoja zinazoonesha matumizi mabaya ya Fedha zilizopelekwa katika Wizara za Afya, Elimu, Utalii, Maji na Watu wenye Ulemavu
Mgawanyo wa hoja za Ukaguzi na Fedha zilizotumika vibaya unaonesha Wizara ya Afya Tsh. Bilioni 91, Wizara ya #Elimu Tsh. Bilioni 33.5, Wizara ya Maji Tsh. Bilioni 82.8, Wizara ya Maliasili na Utalii Tsh. Bilioni 1.2, TASAF Tsh. Bilioni1.5 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Tsh. Milioni 141
Ukaguzi wa CAG ulibaini baadhi ya vifaa ikiwemo Magari yaliyoagizwa kwaajili ya Sekta ya #Afya na Elimu hayakupokelewa kwenye maeneo yalipotakiwa kutumika hadi wakati CAG anamaliza Ukaguzi