KLABU ya YAnga imefanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya timu ya Rivers United ya nchini Nigeria katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kipindi cha kwanza Yanga iliingia ikicheza mfumo wa mabeki watano ambapo upande wa beki wa kushoto alicheza Lomalisa ambaye alikuwa anapanda na kushuka vilevile kwa upande wake Djuma Shabaan.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kuanzia kwenye mfumo kutoka 3-5-2 na kuwa 4-4-2 na kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ambapo mabadiliko hayo yalizaa matunda kwani yalisaidia kupata matokeo hayo.
Pongezi za pekee ziende kwa Nahodha Bakari Mwamnyeto ambaye alitoa pasi za mabao yote mawili ambayo yalifungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele.