Yanga Yaendelea Kushinda Michezo Bila Kocha Nabi


Klabu ya Yanga imemkosa Kocha wake Mkuu, Nasredine Nabi katika michezo yake ya hivi karibuni kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia na timu hiyo kuwa chini ya msaidizi wake, Cedric Kaze.

Yanga ilisafiri kuifuata TP Mazembe nchini Kongo huku ikimkosa Nabi kwenye benchi la ufundi na timu ikafanikiwa kushinda kwa goli 1-0.

Hata hivyo goli la Farid Mussa dakika ya 63 lilikuwa la jasho na damu mpaka kupatikana kwake na kuwafanya Wananchi kuondoka kifua mbele ugenini.

Kwa mara nyingine tena Yanga iliwakabili Geita Gold kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup na kuondoka kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0.

Kama ilivyo kwa Mazembe hata dhidi ya Geita Gold timu ya Yanga ililipata goli hilo moja pekee kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 57 na hali kupatikana kirahisi bali kwa jasho na damu kweli kweli.

Je kutokuwepo kwa Nabi ndani ya kikosi cha Yanga hakuna tatizo katika kupata matokeo ya ushindi kwa Wananchi.?

Imeandikwa na @fumo255

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad