Trevor Jacob (29) Mwana YouTube ambaye aliangusha ndege kimakusudi ili kutazamwa na wafuasi wake mtandaoni anaweza kufungwa hadi miaka 20 jela iwapo atakutwa na hatia kwenye juu ya kesi inayomkabili.
Trevor Jacob alichapisha video ya ajali ya ndege kwenye YouTube mnamo Desemba 2021, na video hiyo Imetazamwa na zaidi ya watu milioni 2.9 hadi sasa.
Katika makubaliano yake na waendesha mashtaka kuhusu kukukiri makosa, alisema alirekodi video kama sehemu ya mpango wake wa udhamini wa moja ya bidhaa.
idara ya haki ya Marekani katika taarifa yake siku ya Alhamisi ilisema, Rubani huyo mwenye umri wa miaka 29 amekubali kukiri kosa moja la uharibifu na kuficha kwa nia ya kuzuia uchunguzi wa serikali.
Mnamo Novemba 2021, Bw Jacob aliondoka kwenye uwanja wa ndege wa Santa Barbara, California kwa ndege ya mtu mmoja huku kamera zikiwa zimepachikwa kwenye ndege yake. Pamoja na kamera, Bw Jacob alikuwa na parachuti, pamoja na fimbo ya kuchukulia picha za 'selfie.
Ndege hiyo ilianguka kwenye Msitu wa Kitaifa wa Los Padres dakika 35 baada ya kupaa. Kabla ya kurudi eneo la tukio la kuchukua picha.
Baadhi ya watazamaji wa YouTube walikuwa na mashaka kuhusu ajali hiyo, wakibaini kuwa Bw Jacob alikuwa tayari amevalia parachuti na hakujaribu kutua kwa usalama.