Ahmed Ally "Yanga Wamefika Fainali Kwa Kucheza na Timu Dhaifu"


Kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Instagram, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema kuwa fainali ya Caf Confederation waliyofikia Yanga ni kwa sababu katika Safari yao ya michuano hiyo walikutana na Timu Dhaifu.

✍🏼 Wamefika fainali kwa kucheza na timu dhaifu zisizokua na uzoefu kwenye mashindano ya Afrika

Group Stage
Mazembe (ICU Wanapulia gesi)
US Monastir (Mara ya kwanza Group Stage)
Real Bamako (Mara va pili Group Stage)

Katika hili kundi hakuna bingwa wa Nchini mwao zaidi ya Mazembe tena alipata ubingwa wa Sandakalawe baada ya As Vita kupokwa points

Robo Fainali
Rivers United, Hii ni Robo Fainali yake ya kwanza ya CAF hajui lolote.

Nusu Fainali
Marumo, Huyu kufika nusu fainali ni tembo juu ya mti, Ndo mara ya kwanza anashiriki mashindano Africa, imagine katika ligi ya kwao amecheza mechi 25 ameshinda nne tuu, Marumo amefika Nusu Fainali kwa sababu Kombe la Shirikisho msimu huu limekua jepesi.

Kwa ufupi ni kwamba hakuna maajabu ambayo UTO amefanya ukitaka kujua kiwango chao halisi cha kimataifa rejea mechi ya Al Hilal.

Wana Simba hatupaswi kuwa wanyonge kwa Fainali yao kwani kwa timu zilizopo Shirikisho hata tungepeleka Simba U20 tungecheza Fainali.

Lunyasi hatujawahi kupata ganda la ndizi kama hili la UTO tangu tumeanza kuusaka ufalme wa Afrika.

Mano msimu huu tuu, Tumecheza na Bingwa wa Malawi, Bingwa wa Uganda, Bingwa wa Morocco, Bingwa wa Guinea na mwisho tukapewa na Bingwa wa Afrika.

Hizi ni njia ngumu ambazo zinazidi kutukomaza

Tuko SITE tunatengeneza timu ya kushindana kwenye mashindano makubwa sio kushindana na wanaoshuka daraja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad