Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreeden Nabi amesema bado inawezekana kwa timu hiyo kupata matokeo ugenini licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 kwenye fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam
Kocha Nabi anasema kama jezi za wachezaji wake zitavuja jasho la mapambano basi inawezekana kupindua meza nchini Algeria
"Najua timu yangu inaweza kupata goli ugenini, tulikwenda Mali tukapata goli, Nigeria tulipata goli, Afrika Kusini pia kwa hiyo tunaweza kupata matokeo," alisema Nabi
Katika hatua nyingine Nabi amesema mchezaji Stephane Aziz Ki alipata majeraha ya mgongo katika mchezo huo, madaktari watatoa taarifa kuhusu maendeleo yake
"Aziz Ki aipata shinda katika mgongo wake, madaktari watamfanyia tathmini na kubaini ukubwa wa changamoto aliyopata"
Aziz Ki jana alionekana kutokuwa katika kiwango bora na alifanyiwa mabadiliko kwenye kipindi cha pili nafasi yake ikichukuliwa na Salum Abubakar 'Sure