Aliyemchangia Figo Selena Gomez Aoga Matusi Kutoka Kwa Mashabiki wa Selena


Mrembo Fransia Raisa ambaye alimchangia Figo moja Mwanamuziki Selena Gomez mnamo mwaka 2017 amezungumza na #Tmz na kueleza masikitiko yake baada ya baadhi ya mashabiki wa #SelenaGomez kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii.
.
Selena na Fransia ni marafiki toka utotoni mambo yakaja kubadilika baada ya Selena kufanyiwa mahojiano baada ya kupandikizwa Figo ya Fransia. Kwenye moja ya mahojiano yake Selena alisema kuwa Mtu pekee ambaye alimjali wakati anasumbuliwa na kufeli kwa Figo alikuwa ni mwanamuziki Tayrol Swift na kusahau kumpa maua yake rafiki aliyehatarisha maisha yake kwa kumpa Figo
.
Jambo hilo lilimkera sana Fransia na kuamua kum-unfollow Selena kwenye mitandao ya kijamii. Sasa toka Fransia afanye hivyo amekuwa akipokea matusi kutoka kwa mashabiki wa Selena jambo ambalo kwa upande wake hapendezwi nalo na limkosesha raha kadri siku zinavyozidi kwenda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad