Amri Kiemba "Sijawahi Kuchukia Kuzomewa Baada ya Kufanya Vibaya"




“Kwa sababu mashabiki ndio ambao wanatushangilia tukiwa uwanjani, mimi sijawahi kukasirika shabiki/mashabiki wanaponizomea. Nazungumzia uzoefu wangu wakati bado nacheza.”

“Mashabiki kuzomea ni ishara kwamba hawaridhishwi na kile ambacho kinafanywa/kinatokea! Kwa sababu wakati wanarishwa na kinachofanywa walishangilia.”

“Hawahawa mashabiki wanaozomea ndio wanapeba picha za wachezaji uwanjani au kujichora majina yao mwilini pindi wanapofanya vizuri.”

“Kwa hiyo ikifika mahali mchezji/wachezaji hawafanyi vizuri mashabiki nao hawana njia nyingine ya kuwasilisha ujumbe zaidi ya kuzomea.”

“Kitu kibaya kwa mashabiki ni kufanya fujo kama kurusha mawe au kuwashambulia wachezaji. Kama wanazomea kuonesha wamechukizwa na jambo sioni tofauti na pale wanaposhangilia wanapofurahishwa na jambo.”

“Mashabiki wametimiza haki yao kwamba, namna mnavyokwenda haturidhishwi, mnapaswa kujitathmini na kutufanya tuwashangilie.”

“Wakati Simba inaenda Mtwara, kila ilipopita kwenye makazi ya watu ilishangiliwa njia nzima na ilipokelewa kwa shangwe kubwa wakati inawasili Mtwara. Kwa hiyo mashabiki pia wanapowazomea wachezaji watu wasione kama wanakosea.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad