ASEC Mimosas Wanatumia Mashindano ya CAF kama jukwaa la kuonesha vipaji vya wachezaji, Kisha Wanawauza



Msimu uliopita ASEC Mimosas walikuwa Kundi moja na Simba kwenye Kombe la Shirikisho la CAF, wakaishia hatua ya makundi. RS Berkane na Simba zikaenda Robo Fainali.

Msimu huu ASEC Mimosas wametoboa hadi Nusu Fainali, wao wanatumia mashindano ya CAF kama jukwaa la kuonesha vipaji vya wachezaji wao na kuwauza. Huo ndio mfumo wao.

Waliuza wachezaji kadhaa ikiwa ni pamoja na Stephane Aziz Ki ambaye alisajiliwa na Yanga. Maana yake msimu huu kuna package mpya imeingia sokoni. Kwa hiyo na hapa tena watauza!

Biashara wanayoifanya sio tu kuuza Ulaya, hata klabu za Afrika wanawauzia wanapiga mpunga maisha yanaendelea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad