Ashitakiwa kwa kuiba viatu vilivyovaliwa katika filamu ya Dorothy

Waendesha mashitaka nchini Marekani wamemshitaki mwanaume kwa kuiba viatu maarufu za rangi nyekundu vilizovaliwa na muigizaji wa filamu ya The Wizard of Oz, Judy Garland akiyecheza kama Dorothy mwaka 1939 .


FBI ilivipata Viatu hivyo vya thamani katika operesheni yake mwaka 2018 – baada ya kuchukuliwa kutoka katika makumbusho mwezi Agosti 2005 – lakini hakuna mtu aliyekamatwa wakati huo.


Jumanne, waendesha mashitaka wa shirikisho, walimshitaki mwanaume wa Minnesota Terry martin, mwenye umri wa miaka 76, kosa la wizi wa kazi kubwa ya sanaa.


Viatu hivyo vilivyopatikana ni moja ya pea nne zilizobakia.


Vilichukuliwa kutoka katika jumba la makumbusho la Judy Garland Museum lililopo Grand Rapids, Minnesota, na mwizi ambaye alivunja kioo na kupitia dirishani na kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma ya jengo.


Hakuna alama za vidole zilizoachwa na hakuna king’ora kilicholia kuashiria wizi, kulingana na shirika la habari la CBC News, ambalo ni washirika wa BBC nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad