Askari wa JWTZ ampiga na kumjeruhi dereva wa basi



Tukio hilo linaelezwa kutokea juzi majira ya saa 1:30 asubuhi katika eneo la Kibaha Kwa Mathias baada ya Shabani (45) aliyekuwa akiendesha basi la Saratoga lenye namba za usajili T 555 DCZ kushambuliwa na kupigwa na askari huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi (ACP) Pius Lutumo, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo. Alisema mtuhumiwa ambaye ni askari wa JWTZ, Koplo Emmanuel Peleka, alimshambulia dereva huyo na kumsababishia kushindwa kuendelea a safari.

Kwa mujibu wa NIPASHE, Kamanda Lutumo alisema kutokana na tukio hilo, Shabani alilazimika kwenda kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Tumbi.

Lutumo alisema chanzo cha tukio hilo ni Koplo Peleka ambaye ni dereva wa gari la jeshi, kujaribu kulipita basi la Saratoga na kuwekewa pingamizi, jambo ambalo lingesababisha ajali, hivyo kusababisha taharuki iliyosababisha gomvi baina yao.

Kamanda Lutumo alibainisha kuwa tayari hatua za kisheria zimechukuliwa kwa kumhoji mtuhumiwa na kupata maelezo ya mwathirika.

Kutokana na tukio hilo, Lutumo alitoa wito kwa madereva kutii sheria za usalama barabarani ili kuepusha taharuki na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusisitiza kuwa mbele ya sheria, wote wako sawa na hakuna aliye juu ya sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad